KAMISHNA MUSSA AKAGUA MIRADI POLISI JAMII PWANI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/24-07-2014
Kamishna MUSSA ALI
MUSSA wa Kamisheni ya Polisi jamii amehitimisha ziara kuzunguka mikoa 20 ya
Tanzania katika mkoa wa Pwani kwa kukagua miradi ya Polisi jamii inayoendeshwa
nchi nzima.
Kamishna MUSSA katika
ziara yake mkoani hapa, ameweza kukagua masuala ya usafiri salama wa bodaboda,
mradi wa usalama wetu kwanza katika shule ya Msingi Miembesaba na kukagua
gwaride la vikundi vya ulinzi shirikishi ya mjini Kibaha.
Akizungumza katika ziara
yake katika mkoa wa Pwani, Kamishna MUSSA ALLY MUSSA amewataka wananchi kujua
tofauti ya Polisi jamii na Vikundi vya ulinzi shirikishi jamii ili kuweza
kupata tafsiri sahihi ya mradi huo.
KAMISHNA MUSSA
amesema kuwa jamii imekuwa ikiamini vikundi vyua ulinzi shirikishi ndio Polisi
jamii, jambo ambalo ni kinyume na falsafa ya uanzishwaji wa Polisi jamii, na
akawaeleza wananchi maana halisi ya ulinzi shirikishi ni kwa kila mmoja wetu
awe mwanamke au mwanaume, mzee au kijana na hata mtoto kuweza kwa njia moja au
nyingine anaweza kuhusika na ulinzi shirikishi.
Katibu wa Polisi
jamii mkoa wa Pwani, BW.PETER MAHABA akisoma taarifa ya kikundi cha ulinzi
shirikishi amesema dhana ya ulinzi shirikishi Polisi katika mkoa wa Pwani
ilianza Machi 15 mwaka 2013 ambapo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani,
Kamishna msaidizi wa Polisi, URLICH MATEI aliitisha makampuni ya ulinzi Mkoa wa
Pwani na hatimaye kupata uongozi uliopo.
BW. MAHABA ameongeza
wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali am,bazo iliwalazimu baadhi ya
watu walioonza nao walijitoa hasa kutokana na mwanzo kuwa mgumu, na wachache
waliopo ndio wanaendelea na mpango huo hadi sasa, na kufanikiwa kupunguza kwa
kiasi kikubwa cha vitendo vya uhalifu.
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Pwani Kamishna msaidizi URLICH MATEI akifafanua amesema wananchi wa
Kibaha wamebadilika na kufanikiwa kupunguza vitendo vya uhalifu kwa
kushirikiana na Polisi jamii, na amewataka wananchi na vikundi vya ulinzi
shirikishi kufanyia kazi kwa vitendo maelezo yaliyotolewa na mkuu wa kamisheni
ya Polisi jamii Kamishna MUSSA ALLY MUSSA.
END.
Comments
Post a Comment