WATOZWA FEDHA KUJIANDIKISHA URAIA PWANI
Ben Komba/Pwani-Tanzania/09-07-2014
Zoezi la kuandikisha wananchi kwa ajili ya
vitambulisho vya uraia limeingia dosari Mkoani Pwani, kufuatia baadhi ya
wenyeviti na watendaji kuwatoza fedha wananchi ambao walifika kwa ajili ya
kujiandikisha.
Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia wakazi wa Kiluvya
“A”, Kata ya Kiluvya Tarafa ya Sungwi wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani ambao
walilalamikia hatua ya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kiluvya “A”, BW.ELISANKA
ELIWARIO kuwatoza shilingi 2000, kwa ajili ya fomu kitu ambacho kilipingwa na
wananchi.
Juhudi za mwandishi wa habari hizi kumfikia Mwenyekiti
huyo wa kitongoji zilizaa matunda kidogo baada ya kujibiwa kwa ufupi, kuwa
fedha wanazochangisha watu ni kwa aji9li ya kutolea kivuli na hata hivyo
akasema hasingeweza kuzungumza zaidi na hivyo nikamuone mtendaji, BI.JUSLINE
MFURU ambaye hakuweza kupatikana kwa kukosa nafasi kutokana na kutingwa na
majukumu.
Baadhi ya wananchi wameeleza kuwa hata pamoja na Ofisa
kutoka NIDA kuwaambia watendaji kuwa zoezi hilo ni bure hiyo haikusaidia na
walivyoondoka nyuma wakaendelea na utaratibu uleule wa kutoza kiasi cha fedha
ili waandikishwe.
Kutokana na hali hiyuo zoezi hilo limeathirika kwa
kiasi kikubwa kutokana na baadhi ya wananchi kutokuwa na kiwango hicho cha
fedha ambacho kikitolewa huwa akina risiti ya kuthibitisha kupokea fedha
zilizotolewa na hivyo kuzua sintofahamu katika jamii.
END.
Comments
Post a Comment