WLAC YANOA WATENDAJI-video
Shirika lisilo la kiserikali linasaidia utetezi wa kisheria kwa wanawake na watoto nchini -WLAC- limetoa mafunzo maalum kwa watendaji wa mahaka, Polisi na Kata katika kuhakikisha wanapanua wigo wa wadau ambao inashirikiana nao katika kuhakikisha malengo yanafikiwa.
Mwezeshaji BI.JANE MAGIGITA shirika hilo limeona vyema kufanya kazi kwa karibu kati yake na watendaji hao muhimu ili kuweza kubadilishana uzoefu na uboreshaji wa utoaji huduma wa kisheria kwa makundi maalum katika jamii yaani wanawake na watoto.
BI.MAGIGITA amefafanua kuwa wanawake na watoto wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali katika maisha yao ya kila siku, ikiwa pamoja na kudhalilishwa kijinsia, uonevu na kudhaurauliwa katika jamii, hivi kuna ila sababu kwa makundi hayo kupatiwa misaada inayohitajika ya kisheria.
Ambapo ameongeza wanawake ndio kundi kubwa linaloishi katika lindi la umaskini mkubwa kutokana na kutopatiwa fursa mbalimbali za kijamii, ikiwa pamoja na mtoto wa kike kutoweza kurithi mali au kumiliki nyumba, hali ambayo kwa sasa hapa kwetu inaanza kupita na wakati.
Mshiriki BI.GRACE TASSO kutoka dawati la jinsia na watoto la Jeshi la Polisi amesema kuwa amegundua kuwa wanawake wengi wamekuwa hawatambui haki zao za msingi na hivyo kufanya jukumu la kuwasaidia kuwa gumu.
BI.TASSO amefafanua kutokana na mafunzo hayo yamempa mbinu mpya ya kuweza kukabiliana na kesi mbalimbali zinazo husiana na wanawake na watoto, ingawa wanawake wengi wanfuata kesi zikiwa katika hatua ya awali kutokana na kurubuniwa wanapokuwa majumbani na kuamua kumaliza kesi nyingi nyumbani ilihali haki ya msingi haipatikana.
na ameshauri wanawake kutokuwa na huruma inapotokea wamewashtaki watu wanawadhalilisha ili kuhakikisha wanakomesha vitendo vyote vinavyokiuka haki za wanwake na watoto.
END.
Comments
Post a Comment