TFF WAPYA WAPONGEZWA
Thursday,
October 31, 2013/Ben Komba/Pwani-Tanzania/17:28:06
Mdau wa soka
mkoa wa Pwani ambaye pia ni kiongozi wa vilabu amewapongeza wajumbe wa kamati
ya utendaji na Rais wapya waliochaguliwa
katika uchaguzi mkuu wa shirikisho la soka Tanzania uliofanyika hivi karibuni.
Akiongea na
mwandishi wa habari hizi mdau mkubwa wa soka katika Mkoa wa Pwani, BW. MRISHO
SWAGALA amewapongeza viongozi wapya waliobahatika kuchaguliwa katika kinyang’anyiro
hicho.
BW.SWAGALA
amefafanua kuwa wanachotakiwa kufanya uongozi mpya ni kutumia fursa hiyo adimu
kunyanyua kiwango cha mchezo wa soka nchini ambao umekuwa ukilegalega siku hadi
siku kwa sababu ya kukosekana viongozi makini.
Aidha ameelezea
Jinsi anavyomjua Rais wa sasa wa TFF, JAMAL MALINZI kama ni mchapakazi wa
ukweli na amemshuhudia mara kadhaa akitumia uwezo wake wa hali na mali kusaidia
mchezo huo hususan katika Mkoa wa Pwani.
END.
Comments
Post a Comment