WAMTAKA RAIS AWASAIDIE MIGOGORO YA ARDHI KIBAHA MJINI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/07-10-2013
Wananchi
mjini Kibaha wamemtaka Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT.JAKAYA
KIKWETE, kuwasaidia katika suala zima la kudhulumiwa viwanja vyao kunakofanywa
na watendaji wa halmashauri ya mji wa Kibaha mkoa wa Pwani kwa kisingizio cha
kupangilia mji.
Mmoja wa wakazi
niliokutana nao, BW.JUMA KOLOKONI MUYOMBO amesema yeye ni mstaafu wa shirika la
elimu Kibaha na mkazi wa Mtaa wa Mkuza ambaye kwa sasa ni mtu wa makamo amekuwa
anamiliki eneo hilo toka mwaka 1977, kiasi cha eka mbili kasorobo.
BW.KOLOKONI
amebainisha kuwa mara baada ya kustaafu aliamua kuendelea kuishi eneo la Picha
ya Ndege na kutumia eneo ambalo anailalamikia halmashauri kama shamba kutokana
na kipindi hicho eneo hilo kuwa pori tofauti na ilivyo sasa.
Naye Mke wa
BW. JUMA KOLOKONI, BI.ASHA NDWELA ameongeza kuwa siku moja akiwa analima eneo
hilo alitokea Mama mmoja ambaye jina lake hakulifahamu na kumtaka aondoke eneo
hilo, kwa sababu eneo hilo ni lake na ameuziwa na halmashauri.
BIBI.NDWELA
baada ya kuona hali hiyo aliamua kwenda idara ya ardhi halmashauri ya mji wa
Kibaha ili kutaka kujua kilichojiri, na ndipo Afisa ardhi aliyejulikana kwa
jina moja la MKOMBO alimwambia kuwa wamekosea kumpatia mama huyo eneo hilo
hivyo akaamua kutoa amri ya kumtaka asiendelee na ujenzi eneo hilo.
BIBI.NDWELA
amefafanua mara baada ya sintofahamu hiyo kupita na Yule Mama kusimamisha
uendelezaji wa eneo hilo, ndipo sasa wakajitokeza watu wengine wanaume ambao walimkuta,
BIBI. NDWELA akiendelea na shughuli zake za kilmo watu wale walikuwa
wanaendelea kuzungukazunguka eneo lake.
Kuona hivyo
BIBI mkubwa huyo aliamua kwenda kuwasalimia na kuwakaribisha lakini kinyume na
matarajio yake, mmoja wa watu wale alimjibu unatukaribisha sisi au
tukukaribishe wewe ikiwa na maana yeye kwa mgeni katika eneo ambalo amelimliki
toka mwak 1977.
BIBI.NDWELA
amefafanua kuwa anachokumbuka yeye kabla ya watu wanaodai wamegaiwa eneo hilo
na halmashauri kujitokeza, kulipita maaofisa wa ardhi wakamwambia kuwa eneo
lake limeingizwa katika mradi wa upimaji viwanja wa SOFU na hivyo mtathimini
angekuja kipindi chochote ili kujua thamani hali ya eno lao, kitu ambacho
hakikufanyika.
Mbali ya
familia hiyo pia kuna, Mkazi mwingine, BW.SEIF MOHAMED naye yupo katika mgogoro
wa ardhi inayochochewa kwa kiasi kikubwa idara ya ardhi halmashauri ya mji wa
Kibaha, ambapo katika hatua ya kushangaza akiwa tayari amejenga nyumba yake na
kuishi miaka 10, alijitokeza mtu akidai hilo ni eneo lake na hivyo kuzua
mtafaruku mkubwa.
BW.MOHAMED
ameongeza kuwa katika kufuatilia haki yake ilifikia hatua alifukuzwa katika
ofisi ya Mkurugenzi wa halamshauri ya mji wa Kibaha kutokana na yeye kuonekena
kuwa kero kutokana na kukazania kudai haki yake ambayo baadaye alifanikiwa
kuipata kwa tabu.
Naye afisa
ardhi halmashauri ya mji wa Kibaha, BW. EDWARD MBALA amejibu tuhuma hizo kwa
kusema BW. JUMA KOLOKONI MUYEMBO alishalipwa fidia kupitia uthamini namba,
KTC/LD/PD/F/80 na kupatiwa kiwanja namba BLOCK
F-115,
ambapo ilimbidi kila mwananchi kulipia shilingi 160,000/= flat rate.
BW.MBALA
ameshindilia kwa kusema kuwa watu hao wlilipwa fidia katika mradi wa viwanja 500
katika eneo la SOFU ambapo uthamini ulifanyika mwak 2005 na fidiA kuanza
kulipwa mwakA 2007 kupitia fedha zilizotolewa kutoka wizara ya ardhi kiasi cha
shilingi milioni 470.
END.
Comments
Post a Comment