RAIS KUZURU MKOA WA PWANI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/2-10-2013/10:21
Raisi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT.JAKAYA MRISHO KIKWETE natarajia kuanza
rasmi ziara yake ya siku nane katika Mkoa wa Pwani,kutembelea kisiwa cha Mafia
hapo kesho.
Akizungumza
na waandishi wahabri ofisini kwake, Mkuu wa mkoa wa Pwani, BIBI.MWANTUMU MAHIZA
amesema kuwa katika ziara hiyo ya kikazi ya siku kati ya mambo ambayo
atayafanya ni pamoja na kupokea taarifa ya mkoa na kuweka mawe ya msingi katika
miradi ya maendeleo.
BIBI.MAHIZA
amebainisha kati ya miradi ya maendeleo itakayowekewa mawe ya msingi ni ya
elimu, afya, mahakama, maji na kuzindua gati la bandari ya Mafia ambalo
litawezesha kisiwa hicho kuweza kufungua milango ya biashara na maeneo mingine.
Aidha mkuu
wa mkoa wa Pwani ameeleza kuwa ziara hiyo itaanzia wilayani Mafia na kuishia
wilayani Bagamoyo ambapo moja ya mambo ambayo yatafanyika ni pamoja na
majumuisho ya ziara nzima.
END.
Comments
Post a Comment