MJUMBE AOMBA KURA TFF
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/24-10-13/10:52
Mgombea wa
nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho la soka nchini kutoka
Kanda namba 11 ya Pwani na Morogoro, anayetoka mkoa wa Pwani RIZIKI MAJALA
ameelezea nia yake ya kufufua soka la Tanzania mara atakapochaguliwa nafasi
hiyo.
RIZIKI
MAJALA ambaye hapo awali alienguliwa katika kinyang,anyiro hicho na hatimaye
jina lake kurudishwa baadaye kama mmoja wa wagombeaji, amebainisha kuanzisha program
maalum ya soka itakayohusisha vijana katika suala zima la kuinua kiwango cha soka.
MAJALA kwa
sasa ni Katibu wa COREFA ambaye mwenye elimu ya chuo kikuu kwenye ualimu,
ameawahi kushika nyadhifa mbalimbali katika vyama vya waamuzi, makocha na soka.
Amejitosa
kugombea ikiwa ni wajibu kwa mikoa ya Pwani na Morogoro kutoa mwakilishi na
amewaomba wajumbe wa mikoa ya Pwani na Morogoro kumpa kura za ndiyo ili
akichaguliwa aungane na wenzie katika kuongoza shirikisho hilo la soka nchini.
END.
Comments
Post a Comment