SUMATRA NA WANANCHI.
Ben Komba/29-Oct-13/10:36:08
AM
Mamlaka way
a usafiri wan chi kavu na baharini SUMATRA wamewasisitizia wananchi kuto
ushirikiano kwao katika kuhakikisha mazingira ya usafirishaji wa abiria na mali
zao unakuwa salama na uhakika.
Afisa mwandamizi
wa SUMATRA mkoa wa Pwani, BW.NASHON IROGA ameyasema alipokutana na waandishi wa
habari ofisini kwake mjini Kibaha ambapo amesema wamekuwa wanakutana na
changamoto mbalimbali wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
BW.IROGA amesema
mara nyingi wamekuwa wakikutana na abiria ambao hawaelewi umuhimu wa magari yao
kukaguliwa, kitu ambacho ni jukumu kubwa la SUMATRA katika kuhakikisha vyombo
hivyo vya usafiri vinakuwa katika
viwango vinavyostahili kusafirsha abiria na mali zao.
Ameongeza
kuwa abiria wengi ulalamika kwamba wanacheleweshwa safari zao ambapo wakati
mwingine mabasi hayo yakionekana dhahiri ni mabovu, na hivyo kuwataka abiria
kuelewa dhana nzima ya SUMATRA ya kukagua magari hayo na kuhakikisha
hayakatishi ruti ambazo yamepangiwa.
Akizungumzia
suala la usafirshaji wa vyombo vya baharini, BW.IROGA amewataka wamiliki wa
vyombo hivyo kuzingatia usalama wa utoaji wa huduma wa safari za majini na
kuwaasa kutodharau maelekezo ya kitaalamu yanayotlewa na mamlaka ya hali ya
hewa kuhusu mwenendo wa bahari.
END.
Comments
Post a Comment