MGOMO WA VYOMBO VYA MOTO VYA MIZIGO
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/21-10-2013/13;30
Madereva wa
Magari madogo ya mizigo,na Pikipiki aina ya Toyo na Bajaj wamefanya maandamano
ya amani kuelekea ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Kibaha
kushinikiza kuwekewa kwa miundombinu katika eneo ambalo wanafanya shughuli zao.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi akizungumza na mmoja wa Viongozi wao, BW.ABDALLAH
ZANDA amesema kitu kikubwa kilichowafanya wachukue hatua ya kuandamana ni
Polisi kuwakamata wakiwa wanatekeleza majukumu yao ya kila siku.
BW.ZANDA
amebainisha kwa kipindi kirefu halmashauri walitoa agizo la magari na pikipiki
za kubeba mizigo kuhama eneo hilo, jambo ambalo wao kwa upande wao hawana
kipingamizi nalo, lakini tatizo ni kukosekana kwa miundo mbinu ya uhakika
katika eneo hilo.
Amefafanua
baadhi ya vitu muhimu ambavyo vinakosekana ni pamoja na huduma ya choo katika
sehemu ambayo inakaa karibu watu 100, mabanda ya mamalishe, kukosekana kwa
mabanda ya kupumzikia madereva na wateja na hivyo kuonekana halmashauri kama
imekurupuka kuanzisha zoezi hilo.
Ofisa
mipango halmashauri ya mji wa Kibaha, BW. JOHNSON NYAMITI amewataka madereva wa
magari madogo ya mizigo na pikipiki hao kuwa watulivu na ameshukuru kukutana
nao na kuwaahidi yale ambayo yoyote wameyalalamikia yatapatiwa ufumbuzi.
BW. NYAMITI
amewaasa madereva kuwekwa kwao pale wasjichukulie kama wametelekezwa bali
halmashauri inafahamu uwepo wao na itahakikisha inaweka kifusi eneo hilo ili
liweze kutumika kipindi chote cha Mwaka.
Comments
Post a Comment