POLISI TARAFA YAANZISHWA PWANI.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/03-10-2013.
Jeshi
la Polisi mkoa wa Pwani limezindua mradi maalum wa Polisi Jamii katika ngazi ya
Tarafa katika kuhakikisha huduma hiyo inafikia katika ngazi ya chini ya jamii
katika kuboresha hali ya ulinzi na usalama.
Kaimu
wa kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani,
Kamishna msaidizi Yusuph Ally alisema kutokana na uanzishwaji wa mradi
wa Polisi jamii ngazi ya Tarafa ambao utawezesha kila Tarafa kuwa na askari 15
ambao watashughulikia na eneo lao.
Kamishna
Msaidizi Ally alifafanua kuwa kupitia utaratibu huo kutawezesha kutanua wigo wa
utoaji huduma kwa jamii na amewataka wananchi kutoa ushirikianao wa hali na
mali kufanikisha mpango huo.
Mratibu
wa mpango wa ulinzi wa shirikishi jamii katika mkoa wa Pwani Inspekta Athumani
Mtasha alisema kwa upande wao wamejipanga kuhakikisha kwa kushirikiana na jamii
wanaanzisha mradi huo kwa manufaa ya suala zima la uzima ulinzi na usalama
katika maeneo yao.
Mtasha
alifafanua kuwa kwa kuanzia, ofisi za mradi huo
zitakuwa kwenye Vituo vidogo vya
Polisi na katika ofisi za watendaji wa mitaa na vijiji wakati utaratibu wa
kupata vituo vya kudumu vya kufanyia kazi.
Akizungumzia
suala la askari ulinzi wa ulinzi shirikishi jamii ambao ni raia kutumia nguvu
wakati wa ukamataji, Mtasha alisema
katika kuhakikisha zoezi hilolinafanikiwa watatoa mafunzo rasmi ya ukamataji
salama ili kuondoa ukiukaji wa haki za
bianadamu.
END.
Comments
Post a Comment