RAIS AZINDUA MRADI WA UMEME VIJIJINI MZENGA
Ben Komba/Pwani-Tanzania/09:55/07-10-2013
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT.JAKAYA KIKWETE amewaasa wananchi wilayani Kisarawe kijiji cha Mzenga katika mkoa wa Pwani kutumia fursa ya usambazaji wa nishati ya umeme vijijini kujiletea maendeleo.
Akiongea na wananchi wa Mzenga DKT.KIKWETE amewahimiza wananchi kutumia nishati ya umeme kujiletea maendeleo endelevu kwa kunanzisha miradi mbalimbali ya uzalishaji mali kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo katika lengo zima la kujikwamua na umaskini.
Aidha DKT.KIKWETE ameelezea imani yake juu ya Waziri anayehusika na Umeme MH.SOSPETER MUHONGO kuhusiana na kuhakikisha mradi huo unaosimamiwa na wakala wa nishati vijijini –REA, RURAL ENERGY AGENCY, unamalizika katika wakati kwa kadri ya malengo ya mradi huo.
Awali Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKT.JAKAYA KIKWETE aliweka jiwe la msingi eneo ambalo mradi huo utatekelezwa ikiwa ni sehemu ya shughuli ambazo amezifanya katika ziara yake katika Mkoa wa Pwani.
Akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wazri wa nishati na madini, MH.SOSPETER MUHONGO amesema wizara yake imetenga jumla ya shilingi bilioni 16.3 kwa ajili ya uzambazaji wa umeme katika vijiji vyote vya mkoa wa Pwani.
Waziri MUHONGO amebainisha kuwa takwimu zinaonyesha katika Mkoa wa Pwani hakuna tatizo la umeme, bali umeme ndiyo unatafuta watu na serikali inachukua juhudi za makusudi kuwataka watu wa mkoa wa Pwani waweke umeme majumbani ili kuweza kufaidika na fursa hiyo.
Waziri MUHONGO ameongeza kuwa ilani ya CCM inasema ifikapo mwaka 2015 inaagiza kuwa asilimia 30 ya Watanzania wanatakiwa kuwa wameunganishwa na umeme wa gridi ya Taifa, jambo ambalo amesema litavuka lengo hilo la ilani ya uchaguzi ya chama hicho.
Mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya millennia, Katika mpango wa usambazaji wa umeme vijijini ulitengewa bilioni 11.2 ambapo transfoma saba zimefungwa, ikiwa pamoja na kusambaza njia za usambazaji za kilometa 28.14,huduma,vijiji vitakavyofaidika ni, Mlandizi,Kikongo, Mzenga A, Mzenga B na Mlandizi.
END.
Comments
Post a Comment