HALMASHAURI YA MJI KIBAHA YAENDELEA KULALAMIKIWA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/29/10/2013-09:41
Halmashauri
ya mji wa Kibaha imeshauriwa kuangalia njia njia mbadala ya kuhakikisha kuwa
pikipiki na wenye magari wanakuwa na maeneo maalum ya kuegesha magari yao.
Hayo
yamezungumzwa na diwani Kata ya Maili moja, BW.ANDREW LUGANO kufuatia
malalamiko ya madereva wa vyombo hivyo kufuatia halmashauri kubandika mabango
kuzuia uegeshaji wa magari maeneo mbayo yamezoeleka kwa shughuli hiyo.
BW.LUGANO
ameongeza kuwa yeye kama diwani wa Kata ya Mailimoja hakubaliani kabisa na
hatua aliyochukua Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kibaha, BI.JENIFA OMOLO
wa kutoa tangazo hilo.
Bw.LUGANO
amemtaka Mkurugenzi kabla ya kuanza kubandika matangazo ya makatazo ya
uegeshaji wa magari na pikipiki maeneo ambayo yamezoeleka, angefanya utaratibu
wa kutengeneza miundombinu ambayo itasaidia kupunguza tatizo hilo yaani
maegesho.
Naye dereva
wa bodaboda BW. RAMADHAN SAID wa mjini Kibaha ameeleza kusikitishwa kwake na
halmashauri kutunga sheria kandamizi kwa wananchi wake kila baada ya muda
Fulani na hali yao imekuwa ya mashaka kutokana na utaratibu wa kiutendaji
kutokuwa makini.
BW. SAID
ameongeza wao wamekuwa wanajitahidi kufuata maelekezo mbalimbali ya maboreshop
yanayotolewa na halmashauri lakini mara zote wamekuwa wahanga wa kukamatwa ovyo
na kulipishwa faini ambazo hazieleweki, wameiomba serikali kuu kuangalia kwa
makini utendaji wa baadhi ya halmashauri nchinio kutokana na baadhi yao
kutumika kuwanyonya wananchi.END.
Comments
Post a Comment