UBADHIRIFU IDARA YA ARDHI.
WANANCHI WADHULUMIWA FIDIA MRADI WA VIWANJA 500 SOFU.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/14:10:2013/11:31
Katika hali inayoonyesha udhaifu mkubwa kwa katika Idara ya ardhi halmashauri ya mji wa Kibaha, mamia ya wananchi walio katika mradi wa viwanja 500 ambao uligharimu fedha za mkopo kutoka wizara ya ardhi wa shilingi milioni 470.
Mmoja wa walalamikaji BW.JUMA MUYOMBE amekana kulipwa fidia yoyote na halmashauri ya mji kuhusiana na ardhi, wakati kwenye kumbukumbu za malipo zinaonyesha kuwa wameshalipwa na hivyo kutumia ujanja kupora maeneo ya wananchi kwa manufaa yao binafsi.
BW.MUYOMBE amesema hatua ya Afisa ardhi halmashauri ya mji wa Kibaha, BW.EDWARD MBALA kudai wananchi wote waliohusika katika mradi wa viwanja 500 vya SOFU kulipwa fidia ni ujanja unaofanywa na baadhi ya viongozi wa halmashauri ili waweze kutumia fedha hizo kwa manufaa yao.
Naye BIBI.ASHA JUMA NDWELA ameshangazwa na hatua ya halmashauri ya miji wa Kibaha, kuonyesha watu mbali eneo lake analomiliki toka mwaka 1977, alipofika mjini Kibaha akiwa mke wa mfanyakazi wa shirika la elimu Kibaha.
AIDHA BI. NDWELA ameshangazwa na hatua ya halmashauri ya miji wa Kibaha mkumuandikia barua ya kutomtambua yeye kama ndio mmiliki halali wa kiwanja kwa miaka mingi na wala halina uhusiano na kiwanja BLOCK F namba 115 ambal;o wao watendaji wa halmashauri wanajaribu kuhalalisha ili kuweza kupora eneo hilo.
Diwani wa Kata ya Mkuza, BW.BOSCHO MFUNDO akizungumzia mgogoro huo amesema kuna matatizo makubwa katika idara ya ardhi katika eneo la mradi wa viwanja 500 vya SOFU, Kutokana na watendaji kujichanganya au wanafanya makusudi kwa malengo Fulani.
Diwani MFUNDO amebainisha kuwa wakati umefika serikali kuwachukulia hatua watendaji wazembe ambao wanatumia madaraka ya vibaya kwa kupora haki za wananchi kwa faida binafsi.
Mradi wa viwanja 500 wa SOFU mpaka sasa ni wananchi 99 tu, ambao wameshalipwa fidia na wengine wakiwa wanazungushwa mpaka sasa bila matumaini yoyote na huku watendaji idara ya ardhi halmashauri ya mji wa Kibaha wakidai wam eshalipa fidia kwa wananchi wote waliohusika na mradi.
END

Comments
Post a Comment