VIDEO-WAMAASAI WAJITOKEZA KUCHANGIA DAMU


Ben Komba/Pwani-Tanzania/14/06/2016 12:01:15

Wananchi jamii ya wafugaji wa Kimasai wametakiwa kutokuwa waoga katika suala zima la kuchangia damu katika vituo vya damu salama ili kuwasaidia wengine wenye mahitaji.

Hayo yamezungumzwa na Msimamizi wa Kituo cha damu salama katika hospitali teule ya rufaa ya mkoa Tumbi, BI.FELICIANA MMASI mara baada ya wananchi hao wa jamii ya ufugaji kutoa damu.

BI. MMASI amebainisha suala la kuchangia damu kwa kabila la Wamasai lilikuwa ni changamoto kubwa na hivyo kuwalazimu kununua damu kutoka kwa watu wengine ili kupatiowa wagonjwa wao wanapopungukiwa na damu.

BI.MMASI ameongeza kuwa mara nyingi watoto wa kimaasai wamekuwa wanakabiliwa na tatizo la upungufu wa damu kutoka na mila na desturi zao za kupendelea vyakula vya nyama na maziwa tu na kuziweka kando mboga za majani ambazo uzalisha damu kwa wingi.

Mchangiaji DAMSSON POLATERI amesema kwa upande wake alikuwa anaogopa kutokana na dhana ambayo ameijenga kichwa kwake kuwa wanaweza kumfyonza damu yote nay eye kufa.

Naye Mchungaji wa Kanisa la GOSHENI, BW. BUKELEBE amebainisha kuwa kwa kushirikiana na kituo cha damu salama alitoa elimu juuu ya uchangiajai wa damu kwa wafugaji hao ambapo amefanikiwa kuwapata hao vijana ambao wamejitolea sambamba na yeye mwenyewe.

END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA