WIKI YA MAZINGIRA YAADHIMISHWA KIBAHA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/01/06/2016 12:31:53

Halmashauri ya wilaya ya Kibaha inaadhimisha wiki ya mazingira kwa kufanya shughuli mbalimbali  zenye kulenga katika kuhakikisha kunakuwepo na mpango endelevu wa utunzaji wa mazingira.

Afisa mazingira halmashauri ya wilaya ya Kibaha, BI. ANNA MULEBA amesema mwaka huu wamejipanga katika kuhamasisha jamii kuelewa kwa upana wake suala zima la mazingira ili kuwepo na utunzaji endelevu.

BI. MULEBA amebainisha kuwa katika kipindi kizima kuelekea maadhimisho ya siku ya mazingira watashirikiana na klabu za wanafunzi za mazingira katika shule za sekondari za Ruvu wanawake, Dossa Aziz na Rfsanjani kupitia vikundi vyao vya ROOTS n SHOOTS.

Na lengo kubwa ni kukifikia kizazi kipya na kukipatia elimu juu ya suala zima la uhifadhi endelevu wa mazingira na utunzaji wa uoto wa asili ili kuhakikisha kizazi kijacho kinakuta mazingira katika ubora wake.


END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA