VIDEO-TASAF YANUSURU KAYA MASKINI KIBAHA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/10/06/2016 17:53:04
Mpango wa
kusaidia kaya maskini wilayani Kibaha katika kipindi cha Mei-Juni mwaka huu
inatarajia kutumia jumla ya Shilingi bilioni 2,768,492,346.42 kwa ajili ya
kuwapatia walengwa ambao wengi wao ni watu wazima na kinamama.
Mratibu wa
TASAF wilayani Kibaha, BW.GOODSON HARRY amesema hayo alipotembelewa na ugeni
kutoka TASAF makao makuu ukiongoozwa na meneja rasilimali watu, BI. TECHLA
MAKUNDI ambaao ulitembelea kushuhudia kupatiwa fedha kwa walengwa katika kijiji
cha Disunyara na Msongola ambapo zaidi ya watu 130 walifikiwa.
Ambapo amesema
serikali kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii-TASAF- inatekeleza mpango wa kunusuru kaya maskini lengo likiwa
ni kukuza uchumi na kupunguza umaskini.
BW.HARRY
ameongeza kuwa kwa sasa TASAF inatekeleza programu ya miradi ya ajira ya
muda kwa kaya maskini katika kipindi cha
kuanzia mwezi Januari 2015 hadi April 2015.
Meneja
rasilimali watu wa TASAF Taifa, BI.TECHLA MAKUNDI amewataka wanufaika
kuhakikisha wanatumia fedha hizo kwa ajili ya kujiletea maendeleo kwa yao na
jamii kwa ujumla wake.
Aidha BI.
MAKUNDI amewaasa wanaofaidika na mpango wa kunusuru kaya maskini kuzingatia
nidhamu ya matumizi fedha.
VOX
1-GOODSON HARRY-MRATIBU TASAF KIBAHA-Mwenye kitenge
VOX 2-TATU
SELEMANI-DED KIBAHA
VOX 3-THECLA
MAKUNDI-Meneja rasilimali watu TASAF makao makuu
END
Comments
Post a Comment