VIDEO-MAANDALIZI SIKU YA MAZINGIRA YAPAMBA MOTO
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/01/06/2016 12:31:53
Halmashauri
ya wilaya ya Kibaha inaadhimisha wiki ya mazingira kwa kufanya shughuli
mbalimbali zenye kulenga katika
kuhakikisha kunakuwepo na mpango endelevu wa utunzaji wa mazingira.
Afisa
mazingira halmashauri ya wilaya ya Kibaha, BI. ANNA MULEBA amesema mwaka huu
wamejipanga katika kuhamasisha jamii kuelewa kwa upana wake suala zima la
mazingira ili kuwepo na utunzaji endelevu.
BI. MULEBA
amebainisha kuwa katika kipindi kizima kuelekea maadhimisho ya siku ya
mazingira watashirikiana na klabu za wanafunzi za mazingira katika shule za
sekondari za Ruvu wanawake, Dossa Aziz na Rfsanjani kupitia vikundi vyao vya
ROOTS n SHOOTS.
Na lengo
kubwa ni kukifikia kizazi kipya na kukipatia elimu juu ya suala zima la
uhifadhi endelevu wa mazingira na utunzaji wa uoto wa asili ili kuhakikisha
kizazi kijacho kinakuta mazingira katika ubora wake.
END.
Comments
Post a Comment