Ben Komba/Pwani-Tanzania/23-07-2013/10:03 Chama cha marefa wilayani Kibaha kinaendesha program maalum ya mafunzo kwa marefa wapya wenye kutaka kujiendeleza kuwa waamuzi katika ngazi mbalimbali za ligi za mchezo huo. Katibu wa Chama cha marefa wilayani Kibaha ambaye pia ndio refa bora wa ligi ya VODACOM msimu uliopita BW.SIMON MBELWA amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwezesha kuzalisha marefa wapya. BW.MBELWA amefafanua kuwa katika mambo ambayo yatazingatiwa katika mafunzo hayo ni ufundishaji wa sheria 17 za soka ambazo kila mwamuzi anapaswa kuzifahamu kwa ufasaha ili kuepusha malalamiko na wakati mwingine hata vurugu katika mchezo huo. Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, BW. GEORGE amesema kwa kupatiwa mafunzo hayo kutawasaidia kufanya maamuzi yaliyo sahihi wakati wakichezesha mechi za michuano mbalimbali. END.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/10/07/2012/16:32:18 FIRE SOCIAL CLUB ya mijini Kibaha imefanya kikao chake cha uchaguzi mkuu na kufanikiwa kupata viongozi watakaoiongoza kwa kipindi cha miaka mitatu, ambapo uongozi huo umenuia kufanya mambo mabalimbali katika kuhakikisha michezo inakuwa ajira ya kutegemewa na vijana. Katika uchaguzi huo Mwenyekiti amechagulia kuwa JUMA MBWANA, na nafasi ya Katibu ikichukuliwa na RICH KIBAJA, Mweka hazina akiwa KESSY PONSI na mtunza vifaa akichaguliwa kuwa ni MESHAKI KAIRA. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Katibu wa FIRE SOCIAL CLUB, RICH KIBAJA amebainisha kuwa lengo ni kukuza michezo hususan timu ya soka ambayo tayari ipo, kwa kuibua vipaji vya vijana ambao wanahitaji usaidizi mdogo ili waweze kusonga mbele katika medani ya michezo. KIBAJA ameongeza kuwa michezo ina umuhimu mkubwa kwa binadamu toka michezo ni starehe, afya na burudani. END
Ben Komba/Pwani-Tanzania/10-Mar-13/18:48:18 Mpango wa wanawake vijana uhuru na maendeleo unaoendeshwa kwa pamoja kati ya ACTION AID na shirika lisilo la kiserikali la YOUTH PARTNERSHIP COUNTRYWIDE -YPC- lenye maskani yake mjini Kibaha limefanikiwa kuwafikia walengwa takriban 400 katika suala zima la kuwapatia wanawake hao vijana elimu juu ya kujitambua na ujasiriamali. Mratibu wa mpango kutoka YPC, BIBI. GROLIA MABERE amesema mpango huo unanuia kuwafikia wanawake vijana 2000 nchi nzima, kwa wilaya ya Kibaha mradi huo umegusa katika halmashauri zote mbili ya mjini na kijijini, kwa kuwakusanya wanawake kutoka katika kata mbalimbali na kuwasaidia kuunda vikundi na kufanya uchaguzi wa viongozi wao. BIBI. MABERE amebainisha kuwa mpaka sasa wamefanikiwa kuwaamsha wanawake vijana na kujitambua na kuweza kushiriki katika mambo mbalimbali ya kitaifa na mtaa ikiwa pamoja na kushiriki chaguzi mbalimbali zinazojitokeza katika maeneo yao. Mratibu huyo wa mpango wa wanawake vijana kutoka YPC...
Comments
Post a Comment