VIDEO-WAWEKEZAJI WA NDANI WAOMBA SERIKALI IWALINDE
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/07/06/2016 10:40:32
Serikali
imetakiwa kuboresha mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kuepusha migogoro kati
ya wakulima na wafugaji nchini.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi, Mwekezaji wa Kimasai katika eneo la Lukenge halmashauri
ya wilaya ya Kibaha, BW.TANONGO MAHENDELO amebainisha kuwa kutozingatiwa kwa
mpango wa matumizi bora ya ardhi kumesababisha kuwepo kwa migogoro isiyo na
lazima.
BW,MAHENDELO
amesema kuwa yeye anamiliki eneo la eka 5000 ambazo ndani yake anahifadhi aina
za miti mbalimbali ambayo kwa hivi sasa ni adimu nchini kutokana na ukataji
holela wa miti kwa matumizi mbalimbali.
BW.MAHENDELO
ameongeza lakini amekuwa akikabiliwa na changamoto za baadhi ya wananchi
wasiozingatia sheria kuvamia katika eneo lake na kuchoma mkaa na anapoamua
kuchukua hatua wanazusha mambo mbalimbali yak um chafua ikiwa pamoja na kudai
kuwa anawatishia na bastola.
BW.
MAHENDELO ambaye ni mfugaji ameweza kusaidia upatikanaji wa maji salama, kuni
na miti ya kujengea kwa wananchi ambao wanafuata utaratibu wa kwenda kwanza kwa
mtendaji wa kijiji na wakipewa barua wanampelekea yeye na kuwapatia huduma
wanayohitaji.
Amekanusha
vikali madai ambayo yametolewa na diwani wa kata ya Magindu kupitia tiketi ya
CHADEMA, BW. SHAABAN MKALI ambaye alidai katika baraza la madiwani la
halmashauri ya wilaya ya Kibaha kuwa mwekezaji huyo amekuwa anawatishia
wananchi kwa bastola wakiingia katika eneo lake.
VOX 1 MWENYE
LUBEGA-MWEKEZAJI MAHENDELO
VOX
2-WASAIDIZI WAKE
END
Comments
Post a Comment