WALALAMIKA WATENDAJI KUWAIBIA
Ben
Komba-Pwani-Tanzania-06/06/2016 10:10:11
Halmashauri
ya wilaya ya Bagamoyo imetakiwa kuwasiliana na Ofisi ya mtendaji wa Kata
inapotokea Mtendaji wa Kijiji ameamua kuhama kituo cha kazi kwa sababu
mbalimbali.
Akizungumza
katika kikao maalum cha Kijiji cha Kitonga kilichopo katika mji mdogo wa
Chalinze, Afisa mtendaji wa Kata ya Vigwaza BW. MASKUZI MASKUZI ambapo amesema
kuwa baadhi ya watendaji wanaohamishwa bila kuwasiliana naye wamekuwa wanaacha
athari kubwa kwa vijiji walivyotoka.
BW.MASKUZI ameongeza
halmashauri kwa kutomshirikisha katika suala uhamisho wa watendaji wa vijiji
inasababisha kuwepo kwa migogoro isiyo na lazima ambayo inazorotesha maendeleo
ya vijiji kwa kuacha makovu ambayo jamii inakuwa vigumu kuyasahau.
Mmoja wa
wananchi KOMREDI NDALO amebainisha kuwa wananchi wanashindwa kuelewa kutokana
na kuhama kiholela kwa watendaji wa kijiji ilihali wakiwa katika kipindi chao
chote hawajawahi kusoma taarifa ya mapato na matumizi na ukiukaji wa taratibu
za utumishi wa umma.
END
Comments
Post a Comment