VIDEO-MKUU WA MKOA WA PWANI KUTOA NENO HITIMISHO LA SIKU YA MAZINGIRA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/04/06/2016 14:25:21
Mkuu wa mkoa
wa Pwani MHANDISI EVARIST NDIKILO kesho anatarajiwa kuwa mgeni wa heshima
katika siku ya hitimishi la wiki ya mazingira ambapo maadhimisho yake
yanatarajiwa kufanyika katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha kimkoa.
Kwa mujibu
wa Afisa mazingira halmashauri ya wilaya ya Kibaha, BI.ANNA MULEBA amesema kwa
sasa wanaendelea na shughuli mbalimbali za usafi ikiwa kufanya usafi eneo la
soko la Mlandizi.
Usafi huo
umefanywa kwa kushirikiana na wanafunzi wa Klabu ya mazingira ya shule ya
sekondari DOSSA AZIZ kupitia kikundi chao kinachoitwa ROOTS AND SHOOTS ambao
wamejitokeza kwa wingi katika kuhakikisha maadhimisho hayo yanafanikiwa.
Bi.MULEBA
amebainisha siku ya hitimisho wanatarajia kufanya usafi ikiwa pamoja na kuzibua
mitaro ya maji machafu kuzunguka mji mdogo wa Mlandizi na maeneo ya jirani na
kauli mbiu ya mwaka huuni ’TUHIFADHI VYANZO VYA MAJI KWA UHAI WA TAIFA LETU’.
END
Comments
Post a Comment