WAMAASAI WACHANGIA DAMU
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/14/06/2016 12:01:15
Wananchi
jamii ya wafugaji wa Kimasai wametakiwa kutokuwa waoga katika suala zima la
kuchangia damu katika vituo vya damu salama ili kuwasaidia wengine wenye
mahitaji.
Hayo
yamezungumzwa na Msimamizi wa Kituo cha damu salama katika hospitali teule ya
rufaa ya mkoa Tumbi, BI.FELICIANA MMASI mara baada ya wananchi hao wa jamii ya
ufugaji kutoa damu.
BI. MMASI
amebainisha suala la kuchangia damu kwa kabila la Wamasai lilikuwa ni
changamoto kubwa na hivyo kuwalazimu kununua damu kutoka kwa watu wengine ili kupatiowa
wagonjwa wao wanapopungukiwa na damu.
BI.MMASI
ameongeza kuwa mara nyingi watoto wa kimaasai wamekuwa wanakabiliwa na tatizo
la upungufu wa damu kutoka na mila na desturi zao za kupendelea vyakula vya
nyama na maziwa tu na kuziweka kando mboga za majani ambazo uzalisha damu kwa
wingi.
Mchangiaji DAMSSON
POLATERI amesema kwa upande wake alikuwa anaogopa kutokana na dhana ambayo ameijenga
kichwa kwake kuwa wanaweza kumfyonza damu yote nay eye kufa.
Naye Mchungaji
wa Kanisa la GOSHENI, BW. BUKELEBE amebainisha kuwa kwa kushirikiana na kituo
cha damu salama alitoa elimu juuu ya uchangiajai wa damu kwa wafugaji hao
ambapo amefanikiwa kuwapata hao vijana ambao wamejitolea sambamba na yeye
mwenyewe.
END
Comments
Post a Comment