VIDEO-YANGA YAPONGEZWA KUFANYA UCHAGUZI WA AMANI
Ben Komba/Pwani-Tanzania/14/06/2016
11:24:44
Mwenyekiti wa
Tawi la Yanga Kibaha kwa mfipa,amepongeza kufuatia kufanya uchaguzi wa amani ambao
umewezesha klabu hiyo kupata viongozi ambao wataongoza katika kipindi hiki.
Mwenyekiti huyo
MRISHO HALFAN SWAGALA amesema hiyo ni hatua muhimu katika kuelekea mafanikio
makubwa ambayo yanaweza kuwa ya aina yake toka kuanzishwa kwa klabu hiyo.
BW. SWAGALA
amempongeza Mwenyekiti YUSSUPH MANJI kwa hatua mbalimbali alizochukua katika
kipindi kilichopita na kuweza kuipatia klabu hiyo mataji matatu na kujenga timu
imara ambayo inaweza kutoa upinzani kwa timu kubwa Afrika.
Aidha amewataka
wanayanga Kujenga umoja klabuni hapo na kuachana na migogoro isiyo na lazima
ambayo inadumaza soka na maendeleo yake klabuni.
VOX-MRISHO
HALFAN SWAGALA
END
Comments
Post a Comment