TASAF YANUSURU KAYA MASKINI KIBAHA


Ben Komba/Pwani-Tanzania/10/06/2016 17:53:04
Mpango wa kusaidia kaya maskini wilayani Kibaha katika kipindi cha Mei-Juni mwaka huu inatarajia kutumia jumla ya Shilingi bilioni 2,768,492,346.42 kwa ajili ya kuwapatia walengwa ambao wengi wao ni watu wazima na kinamama.

Mratibu wa TASAF wilayani Kibaha, BW.GOODSON HARRY amesema hayo alipotembelewa na ugeni kutoka TASAF makao makuu ukiongoozwa na meneja rasilimali watu, BI. TECHLA MAKUNDI ambaao ulitembelea kushuhudia kupatiwa fedha kwa walengwa katika kijiji cha Disunyara na Msongola ambapo zaidi ya watu 130 walifikiwa.

Ambapo amesema serikali kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii-TASAF- inatekeleza  mpango wa kunusuru kaya maskini lengo likiwa ni kukuza uchumi na kupunguza umaskini.

BW.HARRY ameongeza kuwa kwa sasa TASAF inatekeleza programu ya miradi ya ajira ya muda  kwa kaya maskini katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari 2015 hadi April 2015.
Meneja rasilimali watu wa TASAF Taifa, BI.TECHLA MAKUNDI amewataka wanufaika kuhakikisha wanatumia fedha hizo kwa ajili ya kujiletea maendeleo kwa yao na jamii kwa ujumla wake.

Aidha BI. MAKUNDI amewaasa wanaofaidika na mpango wa kunusuru kaya maskini kuzingatia nidhamu ya matumizi fedha.
VOX 1-GOODSON HARRY-MRATIBU TASAF KIBAHA-Mwenye kitenge
VOX 2-TATU SELEMANI-DED KIBAHA
VOX 3-THECLA MAKUNDI-Meneja rasilimali watu TASAF makao makuu


END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA