VIDEO=WANANCHI WATUMIE SHERIA NDOGO KULINDA MISITU

Ben Komba/Pwani-Tanzania/2/12/2016 10:45:20 AM

Wananchi wanaoishi kupakana na msitu wa Ruvu Kusini wametakiwa wasiogope kutumia sheria ndogondogo ambazo wamejiwekea katika suala zima la kulinda misitu ya hifadhi na kuboresha mazingira  yanayowazunguka.

Akizungumza ofisini kwake Meneja misitu  wa Kanda ya mashariki, BW. BAKAR MOHAMED amezungumza hayo alipokutana na waandishi wa Habari ofisini kwake mjini Kibaha amewasisitiza wananchi kutumia sheria zao ndogondogo walizotunga wenyewe katika kulinda misitu ya hifadhi.

BW.MOHAMED ameongeza  kuwa mkanganyiko wa gawio kwenda serikali iwapo wanakijiji wamekamata maharamia wa mazao ya misitu, faini au adhabu  yoyote itatolewa na kamati ya kijiji cha mazingira na fedha kuingizwa katika mfuko wa kijiji.

Toka sheria hizo ndogondogo zzimetungwa kukidhi matakwa ya kijiji husika na hivyo kipato chochote kitachopatikana katika usimamizi wa misitu ya hifadhi hususan ya kijiji hakutakuwa na gawio kupeleka serikali kuu.

Naye BW.YAHYA MTONDA mwakilishi shirika la kuhifadhi misitu ya asili Tanzania amesema kuwa wameona changamoto ikijitokeza juu ya usimamizi wa misitu ya hifadhi kutokana na jamii kushindwa kuelewa mwongozo ambao ulikuwa katika lugha ya kigeni.

BW.MTONDA amebainisha lakini baada ya kupatikana tafsiri rahisi ya mwongozo wa usimamizi shirikishi wa misitu kwa pamoja, wananchi wakaamua kuita kikao cha wadau ili waweze kuelimishana kuhusiana suala zima la ulinzi wa misitu ya hifadhi katika kupunguza hewa ukaa.
Aidha ameishukuru kampeni ya MAMA MISITU kwa juhudi mbalimbali ambayo imefanya katika kuwapatia elimu wananchi juu ya umuhimu wa utunzaji wa misitu ya hifadhi.

MAMA MISITU ni kampeni ya mawasiliano inayolenga kuboresha utawala misitu Tanzania, kukuza matumizi endelevu ya mazo ya misitu ili wananchi waweze kunufaika na rasilimali za misitu na kampeni ya mama msitu imebeba dhamira na maono  ya kuhifadhi, kulinda nakuhamasisha matumizi endelevu ya misitu.

END.


Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA