VIDEO-VIGOGO WAVAMIA MSITU MOROGORO
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/2/27/2016 11:56:43 AM
Wananchi
wamesisitizwa kufuata sheria zilizopo zenye kulinda hifadhi za misitu ili
kuboresha mazingira ya nchi na kuzuia mabadiliko ya tabia ya nchi ambako
kunasababishwa na ukataji hovyo wa miti kwa ajili ya shughuli za kibinadamu.
Mshauri wa
maliasili Mkoa wa Morogoro BW.JOSEPH CHUWA ameyazungumza hayo hivi karibuni
OFISINI KWAKE kufuatia kuongezeka kwa uvamizi wa maeneo ya hifadhi na
kusababisha kuongezeka kwa utokaji wa hewa ukaa ambayo inaathiri majira ya
mwaka.
BW.CHUWA
amesema iwapo kila mmoja wetu akiheshimu sheria za uhifadhi wa misitu kama
ilivyoanishwa kuna uwezekano mkubwa wa kurudisha hifadhi za misitu na kurudi
kama awali.
Moja ya
hifadhi ya misitu iliyovamiwa ni iliyopo kati ya wilaya ya Mvomero na manispaa
ya mji wa Morogoro na watu kuanzisha makazi na wengi wao kuwa ni vigogo wenye
nafasi mbalimbali katika serikali na vyama ikiwa pamoja na matajiri.
Ambapo
kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wananchi wa upande wa Mvomero ambao nyumba
za zimevunjwa kutokana na kujengwa katika eneo la hifadhi, lakini ikiwa tofauti
na wenzao wa manispaa ya Morogoro nao wamevamia na wakiwa wameachiwa kuendelea
kuishi katika hifadhi hiyo kutokana na uwezo wao kifedha na kimamlaka.
Naye mkuu wa
wilaya ya Morogoro, BW. MUHINGO RWEYEMAMU amesema kuwa ofisi yake ina taarifa
ya kuwepo na mgogoro huo na kwa sasa suala hilo lipo mikononi mwa Waziri
anayehusika na ardhi kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi.
Mkuu huyo wa
wilaya ya Morogoro amefafanua kuwa eneo ambalo limevamiwa lilitangazwa kwa
hifadhi toka mwaka 1953.
END.
Comments
Post a Comment