VIDEO-AFISA MTENDAJI ATUKANA KIJIJI KIZIMA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/2/26/2016 3:47 PM
Wanakijiji
wa kijiji cha Kitonga Kata ya Vigwaza wilayani Bagamoyo wamekerwa na tabia ya
afisa mtendaji wa kijiji hicho kutukana wananchi kufuatia mkutano wa wazi ambao
umefanyika kijijini hapo na
kumshirikisha mkuu wa wilaya Bagamayo hivi karibuni.
Wakizungumza
na mwandishi wa RFA Pwani, Mmmoja wa wakazi hao BW.SAID ABDALLAH amesema kuwa amesikitishwa na hatua ya
Mwenyekiti wa Kijiji kushindwa kumchukulia hatua afisa mtendaji huo na kwenda kutoa ushahidi wa uongo mahakamani.
BW.ABDALLAH
ameongeza kuwa baada ya Afisa mtendaji kutukana kijiji kizima na kutishia
kuwakamata kuwapeleka jele kwa ajili ya kwenda kufanywa kinyume na maumbile
hivyo kufanya wazee wa kijiji hicho kutaharuki na kuamua kuchukua hatua za kisheria
ambapo alipofika kule akisaidiwa na mwenyekiti wa kijiji hicho alishinda kesi
kitu ambacho wananchi hawakukubaliana nacho na hivyo kutaka viongozi hao
waondolewe katika nafasi zao.
Kadhia hiyo
imetokea kufuatia mkuu wa wilaya ya Bagamoyo kufanya ziara katika kijiji hicho
na kukutana na malalamiko kuytoka wananchi wakihoji uwajibikaji wa Afisa
mtendaji huyo BW.KESSY ATHUMAN kutokana na kushindwa kuitisha vikao vya
kikanuni kama mwongozo unavyoainisha.
Na ndipo
alipoamua kwenda kuutwika na kuwarudia wananchi anaowaongoza na kuanza
kuwasasambua huku huku akianikiza kwamba atahakikisha anawakamata na kuwafunga
kwa ajili ya kwenda kuingilia kinyume cha maumbile.
RFA ikiongea
na Mwenyekiti wa kijiji cha Kitonga, BW. LAAMECK MSAWANGA amesema yeye kwa upande
wake anasema yeye hakuwepo eneo la tukio siku hiyo na alikuwa nyumbani kwake na
hivyo hata lilipotokea tukio hilo hakujua na amesisitiza kuwaa hivyo alivyosema
hata alipoenda kutoa ushahidi mahakamani.
END.
Comments
Post a Comment