KAMATI ZA MISITU ZAPEWA MENO.


Ben Komba/Pwani-Tanzania/2/7/2016 12:45:29 PM
Wajumbe wa kamati za mazingira wa vijiji vinavyopakana na Msitu wa Ruvu Kusini kutoka wilaya za  Kibaha na Kisarawe zimeunda kamati ya pamoja ambayo itakuwa na wajibu wa kuhakikisha wanashirikiana na ofisi  ya misitu  wilaya katika kuhakikisha mikataba mbalimbali inayohusiana na misitu inatiwa saini kuwa sheria.

Akizungumza katika majumuisho ya mafunzo ya kuchambua mwongozo rahisi wa usimamizi shirikishi wa misitu kwa pamoja  kwa ajili ya ushirikishwaji wa jamii katika usimamizi wa misitu ya hifadhi, BW.CASSIAN SIANGA amesema kupitia kampeni ya MAMA MISITU wameweza kutafsiri mwongozo hu ambao utazipatia kamati za mazingira za vijiji meno.

BW.CASSIAN amebainisha kuwa usimamizi shirikishi wa misitu(USM) ni neno la jumla ambalo linaelezea ushiriki wa jamii katika usimamizi wa misitu, ambapo  kuna aina mbili za ushiriki ambazo ni usimamizi shirikishi wa misitu kwa pamoja ambao unafanywa kwenye ardhi ya misitu ya hifadhi katika ardhi ambayo tayari imeshatengwa na mamlaka na serikali.

Na ameongeza aina ya pili ya usimamizi ni shirikishi wa misitu ambayo hufanyika katika ardhi ya kijiji, katika misitu inayomilikiwa na kusimamiwa na halmashauri ya kijiji kwa niaba ya kijiji na kusababisha uanzishwaji wa misitu ya hifadhi ya kijiji,misitu ya hifadhi ya jamii au misitu binafsi.

Washiriki kwa pamoja walifikia azimio la kuunda kamati ambayo itakwenda kukutana na maafisa misitu wa wilaya ambao kwa njia moja au nyingine wameonekana kuwa kikwazo katika suala zima la kutiwa saini baadhi ya mikataba ya mazingira kutokana na kutumia muda wao mwingi kutumia wakiwa ofisini.


END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA