AFISA MTENDAJI KITONGA BAGAMOYO ATUKANA KIJIJI KIZIMA


Ben Komba/Pwani-Tanzania/2/26/2016 3:47 PM
Wanakijiji wa kijiji cha Kitonga Kata ya Vigwaza wilayani Bagamoyo wamekerwa na tabia ya afisa mtendaji wa kijiji hicho kutukana wananchi kufuatia mkutano wa wazi ambao umefanyika  kijijini hapo na kumshirikisha mkuu wa wilaya Bagamayo hivi karibuni.

Wakizungumza na mwandishi wa RFA Pwani, Mmmoja wa wakazi hao BW.SAID ABDALLAH  amesema kuwa amesikitishwa na hatua ya Mwenyekiti wa Kijiji kushindwa kumchukulia hatua afisa mtendaji huo na kwenda  kutoa ushahidi wa uongo mahakamani.

BW.ABDALLAH ameongeza kuwa baada ya Afisa mtendaji kutukana kijiji kizima na kutishia kuwakamata kuwapeleka jele kwa ajili ya kwenda kufanywa kinyume na maumbile hivyo kufanya wazee wa kijiji hicho kutaharuki na kuamua kuchukua hatua za kisheria ambapo alipofika kule akisaidiwa na mwenyekiti wa kijiji hicho alishinda kesi kitu ambacho wananchi hawakukubaliana nacho na hivyo kutaka viongozi hao waondolewe katika nafasi zao.

Kadhia hiyo imetokea kufuatia mkuu wa wilaya ya Bagamoyo kufanya ziara katika kijiji hicho na kukutana na malalamiko kuytoka wananchi wakihoji uwajibikaji wa Afisa mtendaji huyo BW.KESSY ATHUMAN kutokana na kushindwa kuitisha vikao vya kikanuni kama mwongozo unavyoainisha.

Na ndipo alipoamua kwenda kuutwika na kuwarudia wananchi anaowaongoza na kuanza kuwasasambua huku huku akianikiza kwamba atahakikisha anawakamata na kuwafunga kwa ajili ya kwenda kuingilia kinyume cha maumbile.

RFA ikiongea na Mwenyekiti wa kijiji cha Kitonga, BW. LAAMECK MSAWANGA amesema yeye kwa upande wake anasema yeye hakuwepo eneo la tukio siku hiyo na alikuwa nyumbani kwake na hivyo hata lilipotokea tukio hilo hakujua na amesisitiza kuwaa hivyo alivyosema hata alipoenda kutoa ushahidi mahakamani.


END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA