WANANCHI WALALAMIKA KUBAGULIWA KWA MISINGI YA KISIASA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/2/29/2016 3:04:50 PM
Wananchi katika kijiji cha Kitonga Kata ya Vigwaza Tarafa ya Msoga wilaya ya Bagamoyo wamelalamikia kitendo cha Chama Tawala kuwabagua kwa kufuata misingi ya kisiasa.

RFA imegundua hilo kufuatia kuzuru kijiji hicho cha Kitonga, Ambapo mmoja wa wanachama wa Chama shindani, BW. FADHILI KUNGULWE amesema kuwa kumekuwepo na hujuma mbalimbali ambazo zimekuwa zinfanywa na Chama tawala.

BW.KUNGULE amebainisha kuwa wananchama wa vyama shindani katika kijiji hicho wamekuwa wanaishi katika maisha ya dhiki kufuatia Mwenyekiti wa CCM kijiji cha Kitonga, BW. MOHAMED KIGUMI kutumia nafasi yake kukandamiza wananchi ambao hawaungi mkono chama tawala.

Nilipotaka kujua kwanini wananchi wameigeuka CCM, BW. KUNGULWE amefafanua kuwa kikubwa ni mchakato wa kuwapata wagombea mbalimbali katika uchaguzi mkuu na ikiwa pamoja na kushindwa kuwajibika katika kukiletea maendeleo ya kijiji.

Naye mwananchi mwingine BW,KHALIFA MGALAMO ameongeza kuwa uongozi mzima wa kijiji hicho umeshikwa na ganzi na hasa ukizingatia mpaka sasa kuna vitongoji vitatu kati ya vitano ambavyo havina viongozi toka Juni mwaka jana.

BW.MGALAMO ameongeza wamekuwa wanaongozwa na watu watatu kitu ambacho wamesharipoti kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo bila mafanikio yoyote, na amepinga hatua ya nafasi hizo kushikiliwa kwa muda na wananchama wa CCM, kitu ambacho ni kinyume na utawala bora unaozingatia demokrasia.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA