VIJANA WATAKIWA KUGANGAMALA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/2/21/2016 11:56:15 AM
Mkuu wa
wilaya ya Kibaha BIBI. HALIMA KIHEMBA ameyataka mashirika yasiyo ya kiserikali
kusaidiana na serikali katika kuhakikisha vijana wanatambua wajibu wao.
Ameyasema
wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa utekelezaji wa taasisi ya YOUTH
PARTNERSHIP COUNTRYWIDE katika kipindi cha mwaka 2016/2017 ambao umelenga
katika uhamasishaji wa vijana katika kujitegemea kiuchumi.
BIBI.KIHEMBA
amesema ni wajibu wa vijana wenyewe kuwajibika katika maeneo yao ikiwa pamoja
na kutatua kero zinazowazunguka ikiwa sehemu ya uungaji mkono harakati za Rais Magufuli
katika kuhakikisha Taifa linapiga hatua za maendeleo.
Naye
mwakilishi mkazi wa Taasisi inayosaidia ukuaji wa demokrasia kutoka nchini
Marekani NATIONAL DEMOCRATIC INSTITUTE, BW. BODURIN ADEBO amebainisha kuwa
taasisi hiyo imekuwa ikisaidia mashirika yasiyo ya kiserikali katika masuala
mazima ya utoaji wa elimu ya uraia katika kuimarisha demokrasia na utawala bora
katika maeneo mbalimbali.
Akizungumza
katika uzinduzi huo wa mpango mkakati wa shirika hilo, Mkurugenzi wa YPC,
BW.ISRAEL ILUNDE amebainisha kuwa mwaka huu kipaumbele chao kikubwa itakuwa
kuwawezesha vijana kujikwamua kutoka katika lindi kubwa umaskini
linalowakabili.
Amebainisha
kuwa mbinu ambazo watazitumia ni kuanzisha YPC FOUNDATION ambayo itajihusisha
na kuwapatia mbinu vijana juu ya masuala ya kuweka na kukopa.
END.
Comments
Post a Comment