VIDEO-WANANCHI WASULUBIWA KUTOKANA NA ITIKADI ZA SIASA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/2/29/2016 3:04:50 PM
Wananchi
katika kijiji cha Kitonga Kata ya Vigwaza Tarafa ya Msoga wilaya ya Bagamoyo
wamelalamikia kitendo cha Chama Tawala kuwabagua kwa kufuata misingi ya
kisiasa.
RFA
imegundua hilo kufuatia kuzuru kijiji hicho cha Kitonga, Ambapo mmoja wa
wanachama wa Chama shindani, BW. FADHILI KUNGULWE amesema kuwa kumekuwepo na
hujuma mbalimbali ambazo zimekuwa zinfanywa na Chama tawala.
BW.KUNGULE
amebainisha kuwa wananchama wa vyama shindani katika kijiji hicho wamekuwa
wanaishi katika maisha ya dhiki kufuatia Mwenyekiti wa CCM kijiji cha Kitonga,
BW. MOHAMED KIGUMI kutumia nafasi yake kukandamiza wananchi ambao hawaungi
mkono chama tawala.
Nilipotaka
kujua kwanini wananchi wameigeuka CCM, BW. KUNGULWE amefafanua kuwa kikubwa ni
mchakato wa kuwapata wagombea mbalimbali katika uchaguzi mkuu na ikiwa pamoja
na kushindwa kuwajibika katika kukiletea maendeleo ya kijiji.
Naye
mwananchi mwingine BW,KHALIFA MGALAMO ameongeza kuwa uongozi mzima wa kijiji
hicho umeshikwa na ganzi na hasa ukizingatia mpaka sasa kuna vitongoji vitatu
kati ya vitano ambavyo havina viongozi toka Juni mwaka jana.
BW.MGALAMO
ameongeza wamekuwa wanaongozwa na watu watatu kitu ambacho wamesharipoti kwa
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo bila mafanikio yoyote, na
amepinga hatua ya nafasi hizo kushikiliwa kwa muda na wananchama wa CCM, kitu
ambacho ni kinyume na utawala bora unaozingatia demokrasia.
END.
Comments
Post a Comment