WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA SHERIA NDOGONDOGO ZA MISITU KULINDA HIFADHI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/2/12/2016 10:45:20 AM
Wananchi wanaoishi
kupakana na msitu wa Ruvu Kusini wametakiwa wasiogope kutumia sheria ndogondogo
ambazo wamejiwekea katika suala zima la kulinda misitu ya hifadhi na kuboresha
mazingira yanayowazunguka.
Akizungumza ofisini
kwake Meneja misitu wa Kanda ya
mashariki, BW. BAKAR MOHAMED amezungumza hayo alipokutana na waandishi wa Habari
ofisini kwake mjini Kibaha amewasisitiza wananchi kutumia sheria zao ndogondogo
walizotunga wenyewe katika kulinda misitu ya hifadhi.
BW.MOHAMED
ameongeza kuwa mkanganyiko wa gawio
kwenda serikali iwapo wanakijiji wamekamata maharamia wa mazao ya misitu, faini
au adhabu yoyote itatolewa na kamati ya
kijiji cha mazingira na fedha kuingizwa katika mfuko wa kijiji.
Toka sheria
hizo ndogondogo zzimetungwa kukidhi matakwa ya kijiji husika na hivyo kipato
chochote kitachopatikana katika usimamizi wa misitu ya hifadhi hususan ya
kijiji hakutakuwa na gawio kupeleka serikali kuu.
Naye BW.YAHYA
MTONDA mwakilishi shirika la kuhifadhi misitu ya asili Tanzania amesema kuwa
wameona changamoto ikijitokeza juu ya usimamizi wa misitu ya hifadhi kutokana
na jamii kushindwa kuelewa mwongozo ambao ulikuwa katika lugha ya kigeni.
BW.MTONDA
amebainisha lakini baada ya kupatikana tafsiri rahisi ya mwongozo wa usimamizi
shirikishi wa misitu kwa pamoja, wananchi wakaamua kuita kikao cha wadau ili
waweze kuelimishana kuhusiana suala zima la ulinzi wa misitu ya hifadhi katika
kupunguza hewa ukaa.
Aidha ameishukuru
kampeni ya MAMA MISITU kwa juhudi mbalimbali ambayo imefanya katika kuwapatia
elimu wananchi juu ya umuhimu wa utunzaji wa misitu ya hifadhi.
MAMA MISITU
ni kampeni ya mawasiliano inayolenga kuboresha utawala misitu Tanzania, kukuza
matumizi endelevu ya mazo ya misitu ili wananchi waweze kunufaika na rasilimali
za misitu na kampeni ya mama msitu imebeba dhamira na maono ya kuhifadhi, kulinda nakuhamasisha matumizi
endelevu ya misitu.
END.
Comments
Post a Comment