VIDEO-MAAFISA MISITU WATAKIWA KWENDA NA KASI YA MAGUFULI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/2/7/2016 12:45:29 PM
Wajumbe wa
kamati za mazingira wa vijiji vinavyopakana na Msitu wa Ruvu Kusini kutoka
wilaya za Kibaha na Kisarawe zimeunda
kamati ya pamoja ambayo itakuwa na wajibu wa kuhakikisha wanashirikiana na
ofisi ya misitu wilaya katika kuhakikisha mikataba mbalimbali
inayohusiana na misitu inatiwa saini kuwa sheria.
Akizungumza katika
majumuisho ya mafunzo ya kuchambua mwongozo rahisi wa usimamizi shirikishi wa
misitu kwa pamoja kwa ajili ya
ushirikishwaji wa jamii katika usimamizi wa misitu ya hifadhi, BW.CASSIAN
SIANGA amesema kupitia kampeni ya MAMA MISITU wameweza kutafsiri mwongozo hu
ambao utazipatia kamati za mazingira za vijiji meno.
BW.CASSIAN
amebainisha kuwa usimamizi shirikishi wa misitu(USM) ni neno la jumla ambalo
linaelezea ushiriki wa jamii katika usimamizi wa misitu, ambapo kuna aina mbili za ushiriki ambazo ni
usimamizi shirikishi wa misitu kwa pamoja ambao unafanywa kwenye ardhi ya
misitu ya hifadhi katika ardhi ambayo tayari imeshatengwa na mamlaka na
serikali.
Na ameongeza
aina ya pili ya usimamizi ni shirikishi wa misitu ambayo hufanyika katika ardhi
ya kijiji, katika misitu inayomilikiwa na kusimamiwa na halmashauri ya kijiji
kwa niaba ya kijiji na kusababisha uanzishwaji wa misitu ya hifadhi ya
kijiji,misitu ya hifadhi ya jamii au misitu binafsi.
Washiriki kwa
pamoja walifikia azimio la kuunda kamati ambayo itakwenda kukutana na maafisa
misitu wa wilaya ambao kwa njia moja au nyingine wameonekana kuwa kikwazo
katika suala zima la kutiwa saini baadhi ya mikataba ya mazingira kutokana na
kutumia muda wao mwingi kutumia wakiwa ofisini.
END
Comments
Post a Comment