WAZIRI SIMBACHAWENE AAHIDI KUSHUGHULIKIA KERO SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania2/21/2016 10:28 AM
Shirika la
elimu Kibaha limetakiwa kufanyakazi kwa kadiri ya misingi ya uanzishwaji wake
ili liweze kufikia malengo yalikusudiwa.
Hayo
yamezungumzwa na Waziri wan chi ofisi ya Rais TAMISEMI,BW.GEORGE SIMBACHAWENE
wakati akizungumza akiwa katika ziara ya kutembelea shirika hilo mjini Kibaha.
Ambapo
amesema kuwa kwa kufuta misingi ya kuanzishwa kwake ambako kulikuwa kumelenga
kumkomboa mwananchi wa kijijini kutoka kwa maadui wakuu watatu ujinga,maradhi
na umaskini katika kuhakikisha maendeleo yanafika hadi ngazi ya kijiji.
Aidha katika
ziara yake ametembelea mradi wa mwekezaji ORGANIA ambao wamewekeza katika
mifugo na kilimo na kupata taarifa ya utekelezaji wa mradi huo.
Jambo
jingine ambalo Waziri SIMBACHAWENE alikutana nalo ni malalamiko ya wafanyakazi
ya kuwepo kwa kukosa stahili zao mbalimbali ambapo waziri huyo amewaahidi
wafanyakazi kuzichunguza na kutoa mrejesho kwao hapo uchunguzi utakapokamilika.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Shirika la elimu Kibaha, BW.CYPRIAN MPEMBA amesema shirika
la elimu kupitia hospitali limefanikiwa kuimarisha ukusanyaji wa mapato kutoka
shilingi laki tatu za awali ambazo zilikuwa zinakusanywa kwa siku hadi kufikia
kukusanya shilingi milioni sita kwa siku.
BW.MPEMBA amefafanua
kuwa mafanikio hayo yamepatikana kufuatia kufungwa kwa mfumo wa kielektroniki
wa malipo ambao kwa kiasi kikubwa umepunguza mianya ya upotevu wa fedha.
END
Comments
Post a Comment