VIDEO- HAMAHAMA YATIA FORA


Ben Komba/Pwani-Tanzania/8/22/2015 2:48:56 PM

Katika hatua inayoashiria kuwa vuguvugu la wananchama kimoja kuhamia kingine bado linafukuta kufuatia kuendelea kwa wananchama na viongozi waandamizi katika vyama vya siasa kufanya mzunguko ambapo kuna walioenda mbali zaidi kuzunguka zaidi ya viwili kwa mpigo.

Hali hiyo imeendelea pia wilayani Kibaha ambapo, Mwenyekiti wa CCM Wazazi BW. ALLY BAGO Kata ya Boko Mnemela kuamua kujivua nafasi yake na kujiunga na CHADEMA ikiwa hatua hiyo ameichukua kufuatia kuchukizwa na mambo yanavyoendeshwa katika chama hicho kwa hivi sasa.

BW.BAGO amesema vijana ambao wamepewa vyeo katika chama hicho wamekuwa wapuuzi ambao hawaheshimi wanachama wakongwe ambao wamewakuta katika chama hicho, na amejipanga kufanya kazi na chama chake kipya katika kuhakikisha mabadiliko yanapatikana nchini.

Sawa na tukio hilo la kurudisha Kadi ya chama cha Mapinduzi kwa kada ALLY BAGO ambapo amekabidhiwa kadi ya CHADEMA na Mwenyekiti wa Baraza la wazee wa CHADEMA, BW.PANGISA HAULE, Kulikuwa pia na tukio la kurudisha fomu ya udiwani katika ofisi ya Mtendaji Kata kwa mgombea kupitia tiketi ya CHADEMA, BW.HAMIS JUMA.

BW.JUMA ameelezea kipaumbele chake iwapo akichaguliwa kuwa diwani wa kata kupitia tiketi ya CHADEMA atahakikisha kunakuwepo na shule ya sekondari katika kata ya Boko Mnemela.

END.



Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA