U-MUNGU MTU KUIUA CCM
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/8/11/2015 11:05:47 AM
Mwenyekiti wa
CCM Sumbawanga mjini ametishia kujiuzulu baada ya kuibuka kwa vitendo vya
kukiuka utaratibu wa kura za maoni ya chama hicho katika kupata mgombea ambaye
atawakilisha wananchi wa Jimbo hilo.
Habari za
uhakika ambazo mwandishi wa habari amezipata ni kuwa uongozi wa Chama hicho
wamekuwa wakikiuka taratibu za kura maoni kutokana na wengi wao kuendekeza rushwa na kumbeba mtu anayewapa
chochote.
Mmoja wa
wakazi wa Sumbawanga, BW.HENRY MAKUNGU ameshangazwa na hatua ya CCM mkoa
kutopeleka jina la mmoja wa wagombea kujadiliwa baada ya kukata rufaa kwa lengo
la kumbeba Mbunge amabye amemaliza muda wake, BW.AISHI HILALI.
BW.MAKUNGU
amefafanua kuwa taratibu ambao viongozi hao wa chama kunatoa fursa ya chama
hicho kujimaliza kutokana na baadhi ya viongozi wa chama hicho kujifanya Mungu
watu, kitu ambacho kitakigharimu chama hicho.
Bw. MAKUNGU
ameongeza kutokana na tukio hilo tunajipanga kuhakikisha tunampigia kura
mgombea wa UKAWA, BW SHADRACK MMALILA ambaye ndiye anatarajia kutoa upinzani
mkali kwa mgombea wa CCM.
Habari za
kuaminika zinasema kuwa vitendo hivyo vimesababisha Mwenyekiti wa
CCM,Sumbawanga mjini BW. SULEIMAN KILINDU ametishia kujiuzulu kufuatia
kuporomoka kwa kasi maadili katika chama hicho na kuwathamini watoa rushwa.
Comments
Post a Comment