VIDEO-MAROROSO YA KURA ZA MAONI KIBAHA MJINI


Ben Komba/Pwani-Tanzania/8/6/2015 12:11:35 PM
Wakati wa utaratibu wa kura za maoni za ndani ya Chama Cha Mapinduzi ukiwa umekamilika na huku ukikabiliwa na mapingamizi kibao, Baadhi ya madiwani ambao walijikuta katika uchaguzi uliopita wamepoteza nafasi zao, wamejikuta wakirudi tena kupitia kata mpya zilizoanzishwa.

Baadhi ya maeneo kuna wagombea ambao kwa njia moja au nyingine wamelalamika kuwa kuna wagombea wenzao wamekuwa wananbebwa na viongozi wa Chama wenye jukumu la kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa kufuata misingi ya haki.

Mmoja wa wagombea hao ambaye hakutaka kutajwa jina lake amesema kuwa kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu za uchaguzi kana kwamba tayari kulikuwa na mtu wa ambaye ameandaliwa rasmi na chama.

Ambapo amebainisha kuwa hata baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi huo walikuwa wanafanya mawasiliano ya mara kwa mara na mmoja wa wagombea wa ubunge katika suala zima la kuhakikisha wagombea wa kambi fulani wanashinda.
Zaidi angalia video mwisho kilichofanyika………….
Aidha nimebahatika kuongea na mgombea wa kiti cha udiwani Kata ya Sofu BW.YUSUPH MBONDE ambaye yeye ameshawahi kuwa diwani na kwa mara nyingine amerudia nafasi yake hiyo ya uwakilishi.

Kwa upande wake amesema uchaguzi umeendeshwa kwa haki katika Kata yao na kila mmoja ameridhika na matokeo na hivyo kuwataka wana CCM kuungana ili kuhakikisha kuwa Chama chao kinaibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu ujao.
END


Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA