KURA ZA MAONI CCM ZAZUA MALALAMIKO KIBAHA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/8/2/2015 3:47:54 PM

Wakati wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakimalizia kupiga kura ya maoni kupata wagombea ubunge na udiwani wilayani Kibaha, malalamiko mbalimbali yamejitokeza na hivyo kuendelea kuleta mkanganyiko katika chama hicho kikongwe cha siasa nchini.

Moja ya maeneo ambayo yamezua malalamiko makubwa ni Tawi la Mtambani Mlandizi ambapo wapiga kura ambao ni wanachama wa CCM wapatao 50 walikataliwa kupiga kura hiyo kutokana na majina yao kutoonekana katika daftari ya uandikishaji wa makatibu matawi yao.

Mmoja wa wanachama hao, BI.MARY LUCAS amesema wao wamefika kituoni hapo mapema kupiga kura ili aweze kutumia haki yake ya kikatiba kama mwana CCM, Lakini kutokana na sababu ambazo hakubaliani nazo kutokana nay eye kufuata taratibu zote ikiwa pamoja na kuzikusanya kadi zao na kuzikabidhi kwa makatibu tawi.

BI.LUCAS ameongeza kuwa wamekuwa wakiwauliza wasimamizi wa uchaguzi walikuwa hawana majibu sahihi ya kuwajibu wanachama wao, na kwa upande wake amehuzinishwa na kukosa kupiga kura na hasa ikizingatiwa ni haki yake ya msingi kama mwanachama.

Mwanachama mwingine BI.ZAINAB HATIB amesema kuwa wajumbe walipita katika majumba yao wakakusanya kadi zao za uwanachama kwa takribani mwezi mmoja sasa, anahoji  ni kitu ambacho walikuwa wanafanya.

BI.KHATIB ameelezea mbinu chafu ambazo baadhi ya wagombea wametumia ni kuyabai ni maeneo ambay wao hawana mashabiki na kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa chama wasio waaminifu wamekuwa wanahujumu kwa makusuidi zoezi hilo kwa faida ya baadhi ya wagombea wenye uwezo kifedha.

Naye Bw.FRANK KAGUO amesema yeye ana kadi ya CCM na amekabidhiwa na Katibu wa Tawi wa CCM na kuhakikiwa kama ipo sahihi, lakini cha kushangaza leo hii kunazuka vikwazo ambavyo hajui vimetokea wapi.

Katibu wa uenezi na itkadi wa kata ya Mlandizi wa CCM, BW.AHMED KASSAM amesema wao kwa upande wao, watalifuatilia suala hilo ili kupata ufumbuzi .
END.



Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA