YANGA KUJENGA UWANJA WA KISASA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/8/30/2015 1:10:38 PM
Klabu bingwa
ligi kuu ya Vodacom, Yanga Dar African inaendelea na mchakato wa kujenga
kiwanja cha kimataifa cha michezo katika eneo la Jangwani katika suala zima la
kuhakikisha wanajitosheleza kwenye miundombinu ya michezo.
Mwenyekiti
wa matawi ya Yanga nchini, MOHAMED MSUMI amesema hayo wakati wa uzinduzi wa
Tawi la Yanga Maili moja, Kibaha mjini ambapo amesema kuwa mpaka sasa hatua
mbalimbali zimeshachukuliwa kuhakikisha mafanikio hayo yanafikiwa.
MSUMI
amebainisha kuwa mpaka sasa wameshawasiliana na mamlaka husika ili ikiwezekana
waongezewe eneo la kiwanja chao ili waweze kujenga uwanja huo ambao unatarajiwa
kuchukua mashabiki 40000 na kuwepo kwa vianja mbalimbali kwa ajili kuendeleza
michezo.
Naye mgeni
rasmi katika hafla hiyo mfanyabiashara na mshabiki mkubwa wa Yanga, LLYOD
ATANAKA ameelezea kufurahishwa kwake na hatua hiyo ya wanachama wa Yanga
kujiunga na kufungua Tawi hilo.
Shabiki huyo
wa Yanga,ATANAKA amewasisitiza wanachama hao kutoishia kushirikiana katika
michezo tu, bali hata katika mambo mengine ya kijamii kama sherehe na misiba.
Baadhi ya
matawi ambayo yamehudhuria uzinduzi huo wa tawi la Yanga Mbezi na Tawi la Yanga
facebook community.
END
Comments
Post a Comment