BODABODA WAPATIWA MAFUNZO
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/8/31/2015 4:55:15 PM
Jeshi la Polisi
mkoa wa Pwani limewatunuku vyeti madereva wa bodaboda ambao wamemaliza mafunzo
ya usalama barabarani ambayo yametolewa na shirika lisilo la kiserikali la ANTI
POVERTY AND ENVIROMENTAL CARE-APEC.
Mkurugenzi wa
shirika hilo, BW.RESPICIUS TIMANYWA ameeleza kuwa lengo la mafunzo hayo ni
kuhakikisha usalama wa vyombo hivyo linakuwa jambo la lazima kwa kutoa elimu
ambayo ikizingatiwa itaweza kuokoa maisha ya wengi.
Bw.TIMANYWA
amefafanua kuwa mpaka sasa wameshafikia mikoa 15 katika kuhakikisha wanawajen
gea uwezo madereva kiuchumi na kijamii
na kufanikiwa kupunguza ajali kwa asilimia 95 ya wale ambao wamepatiwa mafunzo.
Mrakibu mwandamizi
wa Jeshi la Polisi TABITHA MAKARANGA amewashukuru APEC kwa kutoa mafunzo hayo
ambayo kwa njia moja au nyingine yataweza kupunguza ajali zinazosababishwa na
bodaboda.
Mrakibu
mwandamizi MAKARANGA amesema kuwa takwimu mpaka sasa zinaonyesha waathirika
wakubwa wa ajali za barabarani ni madereva wa bodaboda.
END
Comments
Post a Comment