MA4ROROSO YA KURA ZA MAONI CCM.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/8/6/2015 12:11:35 PM
Wakati wa
utaratibu wa kura za maoni za ndani ya Chama Cha Mapinduzi ukiwa umekamilika na
huku ukikabiliwa na mapingamizi kibao, Baadhi ya madiwani ambao walijikuta
katika uchaguzi uliopita wamepoteza nafasi zao, wamejikuta wakirudi tena
kupitia kata mpya zilizoanzishwa.
Baadhi ya
maeneo kuna wagombea ambao kwa njia moja au nyingine wamelalamika kuwa kuna
wagombea wenzao wamekuwa wananbebwa na viongozi wa Chama wenye jukumu la
kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa kufuata misingi ya haki.
Mmoja wa
wagombea hao ambaye hakutaka kutajwa jina lake amesema kuwa kulikuwa na
ukiukwaji mkubwa wa taratibu za uchaguzi kana kwamba tayari kulikuwa na mtu wa
ambaye ameandaliwa rasmi na chama.
Ambapo
amebainisha kuwa hata baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi huo walikuwa wanafanya
mawasiliano ya mara kwa mara na mmoja wa wagombea katika suala zima la
kuhakikisha wagombea wa kambi fulani wanashinda.
Zaidi
angalia video mwisho kilichofanyika………….
Aidha
nimebahatika kuongea na mgombea wa kiti cha udiwani Kata ya Sofu BW.YUSUPH
MBONDE ambaye yeye ameshawahi kuwa diwani na kwa mara nyingine amerudia nafasi
yake hiyo ya uwakilishi.
Kwa upande
wake amesema uchaguzi umeendeshwa kwa haki katika Kata yao na kila mmoja
ameridhika na matokeo na hivyo kuwataka wana CCM kuungana ili kuhakikisha kuwa
Chama chao kinaibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu ujao.
END
Comments
Post a Comment