WAANDISHI WA HABARI WAPATIWA MAFUNZO YA UCHAGUZI
Ben Komba/Pwani-Tanzania/8/12/2015 2:26:00 PM
Waandishi 25 wa kutoka kanda ya mashariki odoma ambayo inachukua
mikoa ya Morogoro, Iringa, Pwani na Dodoma wamekutana mkoani
Morogoro kupatiwa mafunzo juu kuripoti ya uchaguzi.
Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Baraza la habari Tanzania na
kufadhiliwa na BBC MEDIA ACTION, Mratibu wa mafunzo hayo kutoka baraza la
habari Tanzania,BW.SAID HASSAN amesma kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea
uwezo waandishi hao katika kuripoti habari za uchaguzi.
BW.HASSAN amefafanua kuwa wameshirikiana na BBC MEDIA ACTION kutoa
mafunzo hayo kwa waandishi hao wamegawanywa katika kanda saba za mafunzo
zikiwemo kanda ya Pwani, Kanda ya Zanzibar, kanda ya Nyanda za juu Kusini,
kanda ya mashariki,kanda ya kati, kanda ya Kaskazini na kanda ya Ziwa.
mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, BI. AGUSTA NJOJI kutoka
Dodoma yeye kwa upande wake ameelezea kufurahishwa kwake na uamuzi wa MCT
na BBC kwa kutoa mafunzo hayo yenye kutoa muongozo kwa waandishi wa Habari kuhusiana
na uandishi wa Habari za uchaguzi.
Bi. NJOJI ameongeza kuwa kutokana na elimu hiyo itawezesha kwa
njia moja na nyingine kuandikwa kwa Habari kuhusiana na uchaguzi kwa umahiri na
weledi wa hali ya juu bila kuegemea upande wowote.
END
Comments
Post a Comment