VIDEO - HAMAHAMA YA VYAMA KIBAHA NAYO HAIPO NYUMANAYO
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/8/22/2015 2:48:56 PM
Katika hatua
inayoashiria kuwa vuguvugu la wananchama kimoja kuhamia kingine bado linafukuta
kufuatia kuendelea kwa wananchama na viongozi waandamizi katika vyama vya siasa
kufanya mzunguko ambapo kuna walioenda mbali zaidi kuzunguka zaidi ya viwili
kwa mpigo.
Hali hiyo
imeendelea pia wilayani Kibaha ambapo, Mwenyekiti wa CCM Wazazi BW. ALLY BAGO Kata
ya Boko Mnemela kuamua kujivua nafasi yake na kujiunga na CHADEMA ikiwa hatua
hiyo ameichukua kufuatia kuchukizwa na mambo yanavyoendeshwa katika chama hicho
kwa hivi sasa.
BW.BAGO
amesema vijana ambao wamepewa vyeo katika chama hicho wamekuwa wapuuzi ambao
hawaheshimi wanachama wakongwe ambao wamewakuta katika chama hicho, na
amejipanga kufanya kazi na chama chake kipya katika kuhakikisha mabadiliko
yanapatikana nchini.
Sawa na
tukio hilo la kurudisha Kadi ya chama cha Mapinduzi kwa kada ALLY BAGO ambapo
amekabidhiwa kadi ya CHADEMA na Mwenyekiti wa Baraza la wazee wa CHADEMA,
BW.PANGISA HAULE, Kulikuwa pia na tukio la kurudisha fomu ya udiwani katika
ofisi ya Mtendaji Kata kwa mgombea kupitia tiketi ya CHADEMA, BW.HAMIS JUMA.
BW.JUMA
ameelezea kipaumbele chake iwapo akichaguliwa kuwa diwani wa kata kupitia
tiketi ya CHADEMA atahakikisha kunakuwepo na shule ya sekondari katika kata ya
Boko Mnemela.
END.
Comments
Post a Comment