SHULE YA JUMUIYA YA WAZAZI CCM KIBAHA HATARINI KUPIGWA MNADA.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/8/23/2015 11:22:24 AM
Iliyokuwa shule
ya Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha Mapinduzi ipo hatarini kupigwa mnada kwa
kudaiwa shilingi milioni 12, ambazo inaelekea Jumuiya hiyo imeshindwa kuzilipa.
Katibu wa
Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Kibaha mjini, BI.ZAITUNI KIOBYA amesema wao
wameshangazwa kusikia kuna gari linapita mitaani likitangaza upigaji mnada wa
shule hiyo ambayo ilijifunga bila utaratibu kutokana na kukosekana kwa
usimamizi madhubuti.
BI.KIOBYA
ameongeza hatua ya kutaka kupiga mnada shule hiyo ulifanyika bila Jumuiya ya
wazazi wilaya kushirikishwa hususan Kamati ya utekelezaji ambayo ndiyo yenye
jukumu la kusimamia shule zote zinazomilikiwa na Jumuiya ya wazazi wa chama cha
mapinduzi.
Amefafanua baada
ya kusikia uamuzi huo wa kutaka kuuzwa kwa njia yam nada kwa shule hiyo,
Jumuiya ya wazazi ikaamua kufuata taratibu za kisheria kuweka pingamizi
kuendeshwa kwa zoezi hilo ambalo lilikuwa liendeshwe na TAMBAZA AUCTION MART,
ambao tayari walikuwa wameweka matangazo yao maeneo mbalimbali.
END.
Comments
Post a Comment