PCCB WAJIPANGA KUDHIBITI RUSHWA YA UCHAGUZI



Ben Komba/Pwani-Tanzania/8/13/2015 10:01:51 PM

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Morogoro imesisitiza kukomesha vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Akiongea na waandishi wa habari ambao walifika  ofisini kwake mjini Morogoro kamanda wa PCCB wa mkoa huo,BW.EMMANUEL KIYABO amebainisha mpaka wamechukua hatua mbalimbali za kukabiliana na rushwa kipindi cha uchaguzi.

Kamanda KIYABO amesema moja ya hatua ambazo wamechukua nikuandaa katazo kuhusiana na utoaji na upokeaji wa rushwa kipindi cha uchaguzi,amebainisha kuwa sababu kubwa ya kuwepo na rushwa katika kipindi hicho tama ya kupata kitu chochote bila kufuata taratibu.

Aidha ameongeza kuwa uelewa mdogo wa wapiga kura kuhusu rushwa na athari zake kipindi cha uchaguzi na hasa kutokana na wananchi kutojua nafasi na wajibu wao katika uchaguzi na umuhimu wa kura zao.

Kamanda huyo wa PCCB mkoa wa Morogoro, BW.EMMANUEL KIYABO ameongeza suala la umaskini ndio unachangia kwa kiasi kikubwa na kusababishwa wananchi kurubuniwa kwa fedha kidogo na kuuza kura zao ili mradi apitishe siku.

Mpaka sasa sheria mbalimbali zimetunghwa kukabiliana na rushwa kipindi cha uchaguzi ikiwa pamoja na sheria za gharama za uchaguzi namba 6 ya mwaka 2010 kwa ajili ya uchaguzi mkuu na sheria ya uchaguzi kwa mamlaka za serikali za mitaa namba 4 ya mwaka 1979.

Waandishi hao ambao kwa sasa wapo katika mafunzo maalum kanda ya mashariki   juu ya kuripoti habari za uchaguzi kwa weledi, kupitia Baraza la habari Tanzania na kudhaminiwa na BBC ACTION FUND.

END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA