MABONDIA KUPAMBANA PWANI NOVEMBA 27 2014-VIDEO
Ben Komba/Pwani-Tanzania/26-11-2014 Kampuni ya GEORGE PROMOTION imeandaa Pambano la ngumi kukata na shoka kati ya Bondia anayechipukia katika mchezo huo mkoa wa Pwani, ZUMBA KUKWE na Bondia mkongwe nchini SWEET KALULU katika pambano ambalo litafanyika kesho Novemba 27 kwenye ukumbi wa Kontena mjini Kibaha. Muandaaji wa mpambano huo, GEORGE NANGAI amesema kabla ya pambano hilo lisilo la ubingwa kutakuwepo na mapambano ya utangulizi ambapo KISOO SOLI atapambana na ISSA NAMPECHECHE, RAMA MAX atapambana na MUSTAPHA DOTTO. Bw. NANGAI amebainisha kuwa lengo la kuaanda mpambano huo ni kunyanyua mchezo wa ngumi katika Mkoa wa Pwani, kwa kutoa fursa kwa vijana kujiajiri katika mchezo huo. END.