WANAKIJIJI WAANDAMANA BAGAMOYO
Ben
Komba/Pwani-Tanzania
Wananchi wa
Kijiji cha Kinzagu kata ya Lugoba Tarafa ya Msoga wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwania
wameandamana kudai utekelezaji wa makubaliano kati ya kijiji na mwekezaji.
Wananchi hao
waliokuwa wakiimba nyimbo za kudai haki zao kufuatia kuchoshwa na ahadi ya
mwekezaji katika madini ya kokoto kijijini hapo kutototekeleza ahadi
walizokubaliana wakati walipofika kuomb ardhi kwa ajili ya uchimbaji wa madini
ya kokoto kwa matumizi ya ujenzi wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa kiji hicho BW. WILLIAM MAKUMU akizungumza kwa niaba ya wakazi amesema kuwa
wanaungana na wanakijiji hao kutokana na Kampuni STRABAG kuchukua ardhi kwa
makubaliano wa ujenzi wa zahanati lakini baada ya kuchelewa kufanya hivyo moja
ya makampuni yanayoenbdesha shughuli za uchimbaji ikajenga hivyo wakaingia
makubaliano mengine ya kuwapatia umeme na kununua trekta.
MAKUMU
amebainisha kuwa Mkandarasi huyo kampuni ya STRABAG imekuwa ikizunguka katika
utekelezaji huo tangu waanze uchimbaji mwaka 2012, hali inayowafanya wananchi
kuwa na imani tofauti huenda viongozi wa kijiji na wa kampuni wanawageuka hali
ambayo haipo.
BW.MAKUMU ameongeza
kuwa mara baada ya kuona suala la zahanati limeshapata ufumbuzi,ndipo mkutano
mkuu wa kijiji ulipoamua kumbadilishia mkandarasi huyo kutoka suala la ujenzi
wa zahanati hadi kutakiwa kununua trekta na umeme.
Mwakilishi wa
kampuni ya STRABAG, BW.JOHN URRASA amewahakikishia wananchi wa Kinzagu kuwa
watulivu nay eye kama mwakilishi wa kampuni hiyo atafikisha ujumbe huo kwa
viongozi wa juu wa STRABAG.
End.
Comments
Post a Comment