CHADEMA WAUNGURUMA VIGWAZA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania
Chama cha
demokrasia na maendeleo kimewataka wananchi katika Mkoa wa Pwani kubadilika na
kuchagua upinzani katika chaguzi zijazo ili kuharakisha maendeleo yao ya
kiuchumi, kijamii na kitamaduni.
Akizungumza
katika ziara yake aliyofanya katika Jimbo la uchaguzi Chalinze, Mbunge wa
Iringa mjini, MCHUNGAJI. PETER MSIGWA amesema tatizo la watu wa Pwani kila siku
kazi yao ni kuchagua watu walewale na hivyo kuwaona wao kama wateja wao.
Na kuwataka
wananchi katika uchaguzi wa serikali ya mitaa kutofanya makosa kuwachagua watu
walewale kwani ni watu ambao hawana uchungu na wananchi wan nchi hii.
Mchungaji.MSIGWA
amesema kuwa kinachoendelea sasa kwa viongozi wa Chama Tawala kuwabeba watoto
wao na kuwapachika nyadhifa mbalimbali na hivyo Chama hicho kukosa sifa ya
kuwaongoza kwa misingi ya haki na usawa na kuamua kuweka mbele maslahi binafsi
badala ya wananchi.
Naye mmoja
wa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Pwani,BW.MBENNA MAKALA amewataka wakazi wa
Ruvu darajani kuyakubali mabadiliko ili kuweza kujiharakishia maendeleo binafsi
nay a Taifa katika ujumla wake.
Ametoa mfano
wake mwenyewe kwa kuweza kuichukua kata ya Tumbi kupitia tiketi ya CHADEMA na
kuiwezesha kata hiyo kwa mara ya kwanza kupata barabara ya Lami ambayo
imesaidia kwa kiasi kikubwa kubadilisha mwonekano wa makao makuu ya mkoa wa
Pwani.
Mara baada
ya kuhutubia wananchi MCHUNGAJI MSIGWA alifungua ofisi ya Chama hicho Kata ya
Vigwaza.END
BW.MAKALA
ameongeza kuwa kwa takriban miaka 50 ya Jimbo la Kibaha kuwa chini ya CCM
hakuna jambo lolote kubwa lenye mashiko ambalo chama imkefanya na hiyvo
kusabisha mambo kuwa shaghalabaghala kiasi cha kushindwa kuuweka mji katika
mpangilio kutokana watendaji waliowekwa na chama tawala kukosa sifa.
Comments
Post a Comment