AJALI ZA PIKIPIKI ZINAVYOMALIZA VIJANA




Ben Komba/Kibah-Pwani/12-9-2014/11:15

Vifo vinavyotokana na ajali za barabarani vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku tatizo linalosababisha mamia kama si maelfu ya vijana kupoteza maisha kunakosababishwa na madereva wazembe.

Mwandishi wa habari hizi katika hali ya kusikitisha alikutana kwa ana na ajali iliyopora maisha ya kijana huyu ambaye alitambulika kwa jina moja tu, La DUCHA akiwa amepata ajali ambayo iliosababisha kupoteza maisha.

Kwa mujibu wa mmoja wa mashuhuda, BW.KINYOGOLI LUSONZO amesema kijana huyo akiwa anatokea kituo cha mabasi Maili moja akiwa upande wake na kwa ghafla akaona gari linakata kona kuelekea upande mwingine wa barabara kana kwamba linamkinga anayekuja na pikipiki.

Kutokana na hatua ya lile gari kukata ghafla kulisabisha pikipiki hiyo kuligonga gari kwa ubavuni na yule kijana kurushwa juu na kichwa chake kupiga lami kama unavyoshuhusidia.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA